Connect with us

Makala

Simba sc Yatambulisha Kocha Mpya

Klabu ya Simba sc imemtambulisha kocha wa zamani wa klabu ya Wydad Casablanca na Petro de Augusto Zoran Manojlović mwenye miaka 59 raia wa nchi ya Ureno kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya kocha Pablo Franco ambaye alitimuliwa klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kutokua na matokeo mazuri.

Kocha huyo inatajwa anapenda kutumia mfumo wa 4-3-3 ambapo timu yake hukaba kuanzia chini kwa lengo la kujilinda zaidi huku akitegemea kushambulia kwa kushtukiza zaidi,amesaini mkataba wa mwaka mmoja kufundisha klabu hiyo yenye makao yake msimbazi kariakoo jijini Dar es salaam.

Rekodi za kocha huyo zinaonyesha kuwa alifundisha klabu vigogo Afrika. Klabu ya kwanza kutaa Afrika kuinoa ilikuwa Primeiro de Agosto kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 akiwa hapo aliifikisha nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya hapo akaenda zake Wydad Athletic Club ya Morocco alidumu kwa msimu mmoja kuanzia mwaka 2019 hadi 2020 na msimu uliofuata akaenda zake Al Hilal ya Sudan.

Safari yake haikuishia hapo kwani Aprili mwaka 2021 alienda kukinoa kikosi cha CR Belouizdad cha nchini Algeria hakukaa sana Agosti 30, mwaka jana akatambulishwa kuwa kocha wa Al-Tai ya Saudi Arabia ambapo alidumu hadi Novemba 4 akatimuliwa kutokana na timu kuwa kwenye nafasi mbaya katika msimamo wa ligi.

“Kocha wetu tayari tumemalizana na amewahi kufundisha klabu kubwa Afrika hivyo ana uzoefu ule ambao sisi tunautaka naTumempa Baraka zote, Simba msimu huu tunataka kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa, mara zote tunaishia robo fainali sasa tunataka kutimiza ndoto yetu ya kwenda nusu fainali”.Alisema moja ya mabosi wa klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala