Connect with us

Makala

Rais Samia Aifanyia Makuu Yanga sc

Baada ya klabu ya Yanga sc kufanikiwa kuingia hatua ya fainali ya kombe la shirikisho nchini baada ya kuifunga timu ya Singida Big Stars kwa bao 1-0 lililofungwa na Fiston Mayele neema zimeendelea kushuka klabuni hapo baada ya Mh.Rais Samia Suluhu kumwaga fedha za maana klabuni hapo.

Iko hivi baada ya Yanga sc kufuzu fainali za kombe la shirikisho barani Afrika ambapo Rais Samia alikua akitoa fedha za hamasa kwa kila goli sasa hamasa hiyo imeongezeka kufikia milioni ishirini kwa kila goli ambalo Yanga sc watashinda katika hatua ya fainali ambapo watacheza Mei 28 dhidi ya Usm Algiers.

Mbali za hamasa hiyo pia Rais Samia amelipia jumla ya tiketi elfu tano kwa ajili ya mashabiki kuingia uwanjani ili kuishangilia klabu hiyo katika mchezo huo wa kihistoria nchini ambapo fainali ya mwisho ilikua mwaka 1993 kwa timu ya Tanzania kucheza.

“Mheshimiwa Rais ameniagiza kuja kuwapa tena pongezi zake za dhati na anawatakia kila la heri kwenye michezo ya fainali na yuko na nyinyi bega kwa bega kuhakikisha tunakamilisha historia hii kubwa kwa kuchukua Kombe” Alisema Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa

Pia Msigwa aliendelea kusema “Tangu tumefuzu kucheza michuano ya kombe la shirikisho imekuwa ni muendelezo wa burudani tangu awali mpaka sasa, nichukue nafasi hii kuwapongeza Viongozi wa Yanga, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki kwa hatua hii tuliyofika, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amenituma niwapongeze, yupo na ninyi na anawatakia kila la heri katika mechi zenu za Fainali”.

Mbali na hayo pia Msemaji mkuu wa Serikali alikabidhi kiasi cha shilingi milioni ishirini za hamasa ambazo zimetokana na mabao mawili waliyoshinda dhidi ya Marumo Gallants ugenini yaliyofungwa na Fiston Mayele na Kennedy Musonda.

“Najivunia sana uwepo wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama ametupa Ndege, ameweka zawadi ya milioni 20 kwenye kila goli lakini kama haitoshi ametoa tiketi Elfu Tano (5,000) kwa mashabiki watakaokuja Benjamin Mkapa Stadium tarehe 28 hii, kwakweli sisi Yanga tunamshukuru sana Mama na tunaahidi kuwa hatutamuangusha” Afisa Habari wa Young Africans SC”Alisema msemaji wa klabu hiyo Ali Kamwe

Yanga sc imekua timu pekee kufuzu hatua ya fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 tangu Simba sc ifanye hivyo mwaka 1993 na itacheza dhidi ya Usm Algiers ambapo mechi ya kwanza itacheza Mei 28 na marudiano yatakuwa June 3 2023.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala