Connect with us

Makala

Paspoti Yamrudisha Brazil Kocha Simba sc

Kocha wa timu ya Simba sc Roberto Oliveira amesafiri kurudi nchini kwao Brazil kwa ajili ya kushughulikia hati yake ya kusafiria baada ya iliyokuwepo kumalizika na kuzua sintofahamu miongoni mwa wadau wa soka nchini.

Kocha huyo amesafiri baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma jiji ambapo mpaka sasa amefanikiwa kuiongoza Simba sc katika michezo miwili ya ligi kuu akishinda yote na hatokuwepo katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Coastal Union ambapo kikosi kitakua chini ya kocha Juma Mgunda.

Kocha huyo licha ya kukaa na kikosi hicho kwa muda mrefu imemlazimu kusafiri kipindi hiki kwani mwezi Februari kikosi hicho kitakua na safari za michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika ambapo kitasafiri katika mataifa mbalimbali kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Simba sc ilimtangaza Robertinho kuwa kocha mpya wa klabu hiyo siku chache baada ya kocha huyo kuvunja mkataba na timu yake ya Vipers Fc ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ambapo siku chache baadae alikwenda kuweka kambi Dubai kwa ajili ya maandalizi ya kikosi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala