Connect with us

Makala

Yanga sc Bado Saba Ubingwa Npl

Endapo klabu ya Yanga sc itafanikiwa kupata ushindi katika michezo saba ijayo ya ligi kuu basi itafanikiwa kushinda ubingwa wake wa ishirini na tisa nchini hasa baada ya kuifunga 1-0 timu ya Ruvu Shooting katika mchezo ulifanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Yanga sc baada ya ushindi huo sasa imebakiwa na michezo tisa pekee ya ligi kuu nchini ambapo michezo saba itacheza Dar es salaa na miwili ikitakiwa kusafiri kwenda Singida kuvaana na Singida Big Stars na mwingine itasafiri kwenda mkoani Mbeya kuifuata Tanzania Prisons.

Hata hivyo Yanga sc  itapaswa kukaza kamba kupata ushindi katika baadhi ya michezo kutokana na uimara wa wapinzani wao hasa michezo dhidi ya Kmc na Namungo Fc mwezi februari huku pia ikiwa na michezo dhidi ya Simba sc na Singida Bigs Stars michezo ambayo endapo watashinda watakua wamepata uhakika wa kuwa mabingwa wa ligi kuu nchini.

Yanga sc tayari msimu uliopita walipata makombe yote nchini huku pia wakifanikiwa kufuzu hatua ya makundi kimataifa katika michuano ya kombe la shirikisho ambapo mwezi ujao wataanza kampeni ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala