Connect with us

Makala

Pamba Jiji Yasajili Dirisha Dogo

Klabu ya Pamba Jiji Fc imekamilisha usajili wa wachezaji wawili kwa mkopo kutoka Singida Black Stars ambao ni Habib Kyombo na Hamad Majimengi ili kujiweka sawa na kurejesha makali yake katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Pamba Jiji ambayo inanolewa na kocha Fred Felix Minziro ipo katika hatari ya kushuka daraja endapo haitafanya vizuri katika duru la pili la ligi kuu ya Nbc nchini ikiwa katika nafasi ya 13 ya msimamo ikiwa na alama 11 katika michezo 13 ya ligi kuu.

Wachezaji hao wanatarajiwa kuja kuongeza kasi hasa eneo la ushambuliaji lililoongozwa na George Mpole.

Wachezaji hao wametolewa kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu ambapo ndipo watarejea Singida Black Stars ili kulinda viwango vyao kutokana na kutopata nafasi ya kucheza kikosini humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala