Connect with us

Makala

Pamba Jiji Fc Yaoga Mamilioni

Klabu ya Pamba Jiji Fc imekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni 10 kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo ikiwa ni hamasa kuelekea mchezo wa kesho ijumaa dhidi ya Yanga sc.

Zawadi hizo zimekabidhiwa na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza na Mwenyekiti wa klabu hiyo Mh.Bhiku Kotecha ambapo mastaa wa klabu hiyo walikua mazoezini kujiandaa na mchezo huo katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

“Tunawashukuru mashabiki kwa kuwa pamoja na sisi katika nyakati zote tulizopitia na tunawaahidi kesho watafurahi kwa kuwa tumejiandaa vizuri”Alisema mchezaji Pauline Kasindi wakatia akizungumzia kuhusu maandalizi ya timu hiyo kwa ujumla kuelekea mchezo huo.

Naye Kocha wa klabu hiyo Fred Felix Minziro alisema kuwa “Tunakutana na timu bora na sisi tutakuja na mbinu mbadala kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huu muhimu”,Alimalizia kusema Minziro.

Pamba jiji itakua na wakati mgumu ikiwavaa Yanga sc ambao wametoka kuifunga Mashujaa Fc mabao 5-0 ugenini mkoani Kigoma.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala