Connect with us

Makala

Pamba Jiji Fc Wapata Ajali

Msafara wa klabu ya Pamba jiji Fc umepata ajali maeneo ya Bahi mkoani Dodoma ukiwa njiani kutokea Bukoba mkoani Kagera kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Kiluvya ambapo basi la klabu hiyo liligonga na roli.

Ajali hiyo imetokea alfajiri saa 10 maeneo hayo baada ya roli la kampuni ya Mwanza huduma kuligonga basi la klabu hiyo pembeni kwa nyuma na kusababisha mshituko Pamoja na michubuko kwa baadhi ya mastaa wa klabu hiyo.

Katika ajali hiyo hakuna majeraha makubwa kwa mastaa wa klabu hiyo ambapo baadhi ya wachezaji wamepata michubuko midogo midogo sambamba na matatizo ya kisaikolojia yaliyosababishwa na mshituko baada ya ajali hiyo.

Pamba jiji Fc ikitokea mkoani Kagera ambapo ilipoteza mchezo wa ligi kuu ya Nbc dhidi ya Kagera sugar ikikubali kichapo cha mabao 2-1 huku siku ya kesho ikitarajiwa kuwavaa Kiluvya United licha ya kupata ajali hiyo.

“ Ni kweli tulipata ajali ambayo mchezaji wetu mmoja aliumia kidogo. Lakini hivi sasa anaendelea vizuri na tunafanya mpango wa kuitoa timu hapa (Ddodoma) iende Morogoro kwa ajili ya mchezo wenyewe” alisema Afisa mtendaji Mkuu wa klabu ya Pamba Ezekiel Ntibikeha

Ntibikeha aliongeza kuwa basi lao ndio limeathirika zaidi na wataliacha Dodoma kwa ajili ya matengenezo kwa gharama za mtu aliyewagonga na wao wataenda Morogoo na usafiri mwingine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala