Connect with us

Makala

Okrah Kuondoka Simba sc

Winga wa klabu ya Simba sc Augustine Okrah amemalizana na klabu ya Simba sc na kwa kufikia makubaliano ya kuondoka klabuni hapo baada ya benchi la ufundi la klabu hiyo kutoridhishwa na mchango wake katika timu hiyo.

Iko hivi,staa huyo alisajiliwa klabuni hapo huku mabosi wakiwa na matarajio makubwa kuwa atafanya mambo makubwa huku akibebwa zaidi na takwimu zake za msimu uliopita akiwa nyumbani kwao nchini Ghana katika klabu ya Bechem United akicheza michezo 32 na kufunga mabao 14 huku akicheza kama winga wa kulia.

Hata hivyo baada ya kujiunga na Simba sc kwa mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwingine zaidi,kocha Roberto Oliveira ameonyesha kutoridhishwa na kiwango cha staa huyo ambaye muda mwingi alikua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Pia ripoti za ndani zinadai pia Okrah hakua na mwenendo mzuri nje ya uwanja ambapo mara kadhaa alikutwa na matatizo ya utovu wa nidhamu huku ikitajwa kuwa klabu ya Singida Big Stars imeulizia kuhusu huduma ya mchezaji huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala