Connect with us

Makala

Nyuma ya Jeuri ya Onyango Simba sc

Inasemekana kwamba beki wa klabu ya Simba sc Joash Onyango amegoma kuongeza mkataba klabuni hapo akihitaji kulipwa mshahara wa dola elfu tano kwa mwezi huku akihitaji dau la usajili linalokadiriwa kufikia milioni mia na ishirini ili asaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuchezea klabu hiyo.

Simba sc ilimsajili Onyango kutoka Gormahia Fc ya nchini Kenya misimu miwili iliyopita na tayari beki huyo ameonyesha ustadi mkubwa hasa katika kupambana na washambuliaji wakorofi na wenye kasi kama Tuisila Kisinda na Fiston Mayele huku pia akijihakikishia namba mbele ya mabeki wenzie klabuni hapo.

Jeuri ya kwanza ya Onyango katika dili hilo inatokana na ukweli kwamba kwa sasa ana uhakika wa namba klabuni hapo kutokana na uwezo aliouonyesha kumkosha kocha Pablo Franco ambaye humpanga yeye pamoja na Henock Inoga Baka huku Pascal Wawa na Kennedy Juma wakilazimika kusubiri benchi.

Pia beki huyo ameonyesha ukomavu wa hali ya juu hasa katika suala la nidhamu uwanjani hasa akiepuka kadi nyekundu ambazo hazina msingi tofauti na wenzake Wawa na Inonga ambao nidhamu ya uwanjani na nje ya uwanja hasa kwa Wawa imekua tatizo kubwa.

Ofa kubwa alizonazo beki huyo kutoka vilabu vya Afrika ya kusini pia ni sababu nyingine ya kuhitaji dau kubwa ili kubaki Msimbazi ambavyo inasemekana vilabu vya Mamelod Sundowns na Kaizer Chiefs vinafuatilia kwa ukaribu mkataba wa mchezaji huyo.

Onyango alisajiliwa na Simba sc misimu miwili iliyopita kutoka klabu ya Gormahia Fc ya nchini kwao aliyoichezea kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuitwa mara kwa mara kuichezea timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee stars’.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala