Connect with us

Makala

Ntibanzokiza Anukia Simba sc

Inasemekana aliyekua kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza ameanza mazungumzo kujiunga na klabu ya Simba sc baada ya kushindwana na klabu ya Yanga sc kuhusu kusaini mkataba mpya.

Inadaiwa kwamba Simba sc ipo tayari kumpatia staa huyo mkataba wa miaka miwili kama anavyotaka ili ajiunge na mabingwa hao mara 18 wa ligi kuu nchini na wametumia kipindi hiki akiwa na timu ya Taifa ya Burundi kufanya mazungumzo hayo ya kujiunga na klabu hiyo na yameenda vizuri huku kwa upande wa klabu ya Yanga sc nao wamegawanyika kuhusu kumtema staa huyo huku suala la usajili wa Caf kumalizika juni 30 limeanza kufufua matumaini ya klabu hiyo kumfikiria mchezaji huyo kwa hofu ya kutokamilisha usajili kwa muda uliopangwa na Caf wa 30 juni.

Mbali na Simba sc pia klabu ya Azam Fc inadaiwa kumfikiria kumsajili staa huyo ili kuongeza uzoefu kikosini humo kwani wamepanga kushusha mastaa wa kimataifa wa nguvu wakiwa na matumaini ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao baada ya Tanzania kupata uhakika wa kuingiza timu nne.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala