Connect with us

Makala

Gadiel Atua Singida All Stars

Beki wa klabu ya Simba sc Gadiel Michael ambaye yupo katika orodha ya kutemwa klabuni hapo inasemekana tayari amefikia makubaliano ya kujiunga na timu ya Singida All Stars ambayo imepanda daraja kwenda ligi kuu msimu ujao.

Awali timu hiyo ilijulikana kama Dtb lakini hivi karibuni imebadilisha jina na kuitwa Singida All Stars huku ikiwa na mapango kabambe wa kushusha mastaa wa maana kwa ajili ya kuwasajili kwa msimu ujao wa ligi kuu na imeanza mazungumzo na mastaa hao akiwemo Gadiel ambaye hana namba katika kikosi cha Simba sc.

Mchezaji huyo anayecheza pembeni kushoto amekua na wakati mgumu tangu ajiunge na Simba sc akitokea Yanga sc akikosa namba mbele ya Mohamed Hussein na alikua katika hatihati ya kutemwa toka msimu uliopita wa ligi kuu na tayari inasemekana yupo katika orodha ya watakaotemwa msimu huu na klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala