Connect with us

Makala

Ninja Ajifunga Yanga Miaka Miwili

Beki wa kati Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ amesaini dili la miaka miwili leo Agosti 6 kuitumikia klabu ya Yanga akitokea MFK Vyskov ya Serbia.

Ninja alirejea nyumbani Tanzania baada ya kukosa nafasi ya kikosi cha kwanza ndani ya MFK Vyskov na alianza majaribio ndani ya Yanga chini ya Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga ambaye amefutwa kazi Julai 27.

Hatimaye leo beki huyo ametambulishwa rasmi kurejea kwenye timu yake ya zamani na huu unakuwa ni usajili wa tano kwa Yanga ambayo ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala