Connect with us

Makala

Ni Furaha Tupu ,Real Madrid

Real Madrid iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zinadine Zidane imejishindia taji la La Liga la 34 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Villareal uliochezwa Uwanja wa Alfredo do Stefano.

Mabao yote mawili yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 29 na lile la ushindi lilipachikwa dakika ya 77 kwa mkwaju wa penalti huku bao kutoka Villarreal lilifungwa na Vicente Iborra dakika ya 83.

Madrid imetwaa taji hilo ikiwa imeshinda jumla ya mechi 10 mfululizo jambo linalowafurahisha mashabiki pamoja na benchi la ufundi la Real Madrid kwani  imetwaa ubingwa ikiwa imebakiza mechi moja mkononi na ina pointi 86 ambazo hazitafikiwa na mpinzani wake Barcelona mwenye pointi 79.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala