Connect with us

Makala

Mzamiru Kuikosa Yanga Sc

Kiungo wa klabu ya Simba Sc Mzamiru Yassin anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili ili kujitibu majeraha yake ya kisigino yanayomsumbua.

Mzamiru aliumia katika mazoezi ya klabu hiyo na hivyo kumfanya awe chini ya jopo la madaktari wa klabu hiyo.

Kutokana na majeraha hayo mchezaji huyo anatarajiwa kuikosa mechi baina ya klabu yake na Coastal Union itakayofanyika machi mosi mkoani Arusha pamoja na ile ya machi 8 2025 dhidi ya Yanga sc itakayofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unaotarajiwa kutoa hatma ya ubingwa wa ligi kuu ya Nbc nchini kwa kawaida huvutia mastaa wengi kutaka kucheza ili kuonyesha uwezo wao pamoja na kupata mgao mkubwa wa fedha mbalimbali ambazo hutolewa kama bonansi kwa mastaa wa klabu hizo.

Hata hivyo pamoja na majeraha bado hata akiwa fiti Mzamiru amekua hachezi mara kwa mara klabuni hapo baada ya kusajiliwa kwa Deborah Fernández na Yusuph Kagoma ambao hucheza pamoja na Fabrice Ngoma katika eneo la kiungo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala