Connect with us

Makala

Mwalimu Ajiunga Rasmi Wydad Athletic

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Wydad Athletic Club Selemani Mwalimu tayari ameondoka nchini kuelekea nchini Morocco kujiunga na kambi ya timu hiyo rasmi.

Siku chache zilizopita Wydad Athletic ilitangaza kumsajili staa huyo kutoka klabu ya Singida Black Stars kwa dau la takribani milioni mia nane na ushee.

Mwalimu anajiunga na Wydad Athletic kama mchezaji wa timu ya vijana ambapo atakua anacheza pia na timu ya wakubwa chini ya kocha Rulani Mokwena.

Mokwena aliamua kumsajili Mwalimu baada ya kumkosa Clement Mzize ambaye klabu yake ya Yanga Sc ilihitaji dau kubwa kumuuza kwa kipindi cha dirisha kubwa la usajili.

Mwalimu anakua mchezaji wa tatu nchini kuzichezea klabu za Morocco akianza Simon Msuva na Nickson Kibabage ambao waliichezea Diffaa El Jadid kabla ya Msuva kujiunga na Wydad Athletic Club.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala