Simba sc ipo mbioni kumalizana na kiungo wa zamani wa klabu ya Azam Fc Mudathir Yahya Abbas kuijunga na klabu hiyo kama mchezaji huru baada ya kuachana na klabu yake ya Azam Fc mwanzoni na msimu huu.
Simba sc inamsajili staa huyo ili kuchukua nafasi ya Victor Akpan na Nassoro Kapama ambao wameshindwa kuwa na mchango mzuri kikosini hivyo kufikiria namna ya kuchana nao ikiwemo kuwatoa kwa mkopo kwenda vilabu vingine ama vya ndani ama nje ya nchi.
Mudathir inasemekana tayari ameshakubaliana na matajiri wa Simba sc kujiunga nao ikiwemo kukubaliana maslahi binafsi na mchezaji huyo na muda wowote anaweza kusaini na kutambulishwa kikosini humo.
Kwa chanzo cha taarifa hii kutoka ndani ya klabu ya Simba sc kilikua na haya ya kusema kuhusu usajili huo ambao baadhi ya wadau wa klabu hiyo kama wanautilia mashaka.
“Ni kiungo mzuri atakuja kuongeza kitu ndani ya timu uwepo wa Sadio Kanoute, Jonas Mkude na Mzamiru Yassin, hauwezi kuondoa kuongezwa wachezaji wengine kwani Simba ni timu kubwa ina mashindano mengi pia kuna kuumia kwa mchezaji, hivyo lazima mbadala awepo ambaye pia ana kiwango kikubwa,” kilisema chanzo hicho.
“Hili ni dirisha la usajili ambalo lipo kwa ajili ya kuboresha kikosi kutokana na kile kilichofanyika kwenye michezo ya mwanzoni mwa msimu, kocha kapendekeza ongezeko la mchezaji eneo hilo hatujakurupuka.