Connect with us

Makala

Mtibwa Yafungiwa Kusajili Fifa

Klabu ya Mtibwa Sugar imefungiwa kusajili na Shirikisho la soka Duniani (Fifa) kutokana na kutokamilisha malipo ya fedha za usajili za mchezaji Justin Ndikumana ambaye ilimsajili klabuni hapo msimu uliopita.

Fifa iliwataka Mtibwa Sugar kulipa kiasi kinachokadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 34 za kitanzania ambapo walipewa siku 45 kukamilisha malipo hayo.

Sasa rasmi baada ya Mtibwa Sugar kushindwa kukamilisha malipo hayo sasa wamefungiwa rasmi kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Fifa na nakala yake kupatiwa wahusika.

Mtibwa Sugar wamefungiwa kusajili wachezaji wa ndani pamoja na wale wa kigeni mpaka hapo watakapolipa kiasi hicho tajwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala