Connect with us

Makala

Mo Aingilia Usajili wa Beki

Tajiri wa klabu ya Simba sc ameongeza nguvu katika usajili wa beki wa Cotton Sports ya nchini Cameroon Che Fondoh Malone ili atue msimbazi kusaidiana na Henock Inonga katika eneo la ulinzi la klabu hiyo.

Awali Simba sc walipeleka ofa ya dau la usajili la dola elfu arobaini ambalo limekataliwa na klabu hiyo wakidai halitoshi wakitaka walipwe kiasi cha dola laki na hamsini ili wamuachie beki huyo mwenye akili ya mpira na mwili wa mazoezi.

Sasa tayari Simba sc imewasilisha ofa ya pili ambayo ni dola elfu sabini ikiwa takribani ni nusu ya dau wanalohitaji klabu yake huku inasemekana kuwa tajari wa klabu hiyo Mohamed Dewji amewataka kuhakisha kuwa beki huyo anasajili haraka kutokana na klabu hiyo kuwa na bajeti ya usajili tayari.

Simba sc inapambana kukamilisha usajili wa beki huyo ili wamuache Joash Onyango ambaye ameomba kuondoka klabuni hapo mara kadhaa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala