Connect with us

Makala

Mgunda Ashindwe Mwenyewe

Mabosi wa klabu ya Simba sc wamempa kocha Juma Mgunda huduma sawa na wanazopewa makocha wa kigeni wakiwemo kina Zoran Maki na Didier Gomez walipokua wakiifundisha klabu hiyo kwa nyakati tofautitofauti baada ya kumpatia nyumba na gari ya kutembelea pamoja na dereva.

Nyumba hiyo aliyopewa Mgunda ina hadhi kubwa na ipo karibu na bahari huku pia akipewa gari kali aina ya Tata ambayo ataitumia mazoezi na katika misafara rasmi ya klabu hiyo ili kumpa hadhi sawa na makocha wa kigeni na kumtuliza akili ili aifanye kazi yake ipasavyo.

Mabosi wa klabu ya Simba sc wameamua kufanya hivyo ili kumpa morali pamoja na kuhakikisha anafanya maamdalizi mazuri kuelekea mchezo dhidi ya Premero De Augosti ya Angola na michezo ya ligi kuu nchini huku wakitaka kuhakikisha mpaka januari wawe wamepata kocha mpya ambaye atakuta timu imeandaliwa vyema na Mgunda.

Kocha huyo amejiunga na Simba sc kama kocha wa muda akitokea klabu ya Coastal Union kuja kuchukua nafasi ya kocha Zoran Maki ambaye alikubalina na uongozi wa klabu hiyo kuvunja mkataba kwa maslhai ya pande zote mbili na kwenda kujiunga na klabu ya All Ittihad ya nchini Misri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala