Connect with us

Makala

Bosi Mpya Atambulishwa Yanga sc

Klabu ya Yanga sc imemtambulisha Mr Andre Mtine kuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Senzo Mazingiza ambaye aliamua kutoongeza mkataba klabuni hapo baada ya kuhudumu kwa miaka miwili akitokea klabu ya Simba sc iliyomtoa Afrika Kusini.

Mtine katika wasifu wake amefanikiwa kufanya kazi katika klabu ya soka ya Tp Mazembe pamoja na katika Shirikisho la soka barani Afrika(Caf) huku akiktumia chama cha soka cha nchini Zambia pamoja na klabu ya Power Dynamo ya nchini humo.

Bosi huyo ametambulishwa leo na Rais wa klabu hiyo Eng.Hersi Said mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema kuwa “Tunafahamu katika mfumo wa sasa CEO ndiye mtendaji mkuu wa klabu yetu, wiki kadhaa tulitangaza nafasi hiyo na tuliteua kamati ndogo ya kupitia maombi hayo na leo kwa heshima kubwa tunamtangaza CEO wa Klabu yetu Bwana Andrew Mtine”.

Naye Bosi huyo mpya ambaye alivaa suti ya gharama katika utambulisho huo alisema kuwa “Ni heshima kubwa kuwa mtendaji mkuu wa Yanga, najua Yanga Sc ina historia kubwa ndio maana nimechagua kufanya kazi hapa, natambua nafasi kubwa ya wale wote ambao wamefanya kazi kubwa kufikisha Yanga hapa ilipo”.

UZINDUZI WA NJIA MPYA ZA MAPATO:

Pia katika mkutano huo pia Yanga sc imetambulisha vyanzo vipya vya mapato ambapo imezindua rasmi website ya klabu pamoja na Applikesheni mpya ya simu inayopatikana katika simu janja zote mabapo wanachama watakua na uwezo wa kupata taarifa mbalimbali za klabu pamoja na kujisajili katika mfumo wa kielektronika kupitia simu yake ya mkononi.

“Huu ni muendelezo wa ajenda yangu kubwa katika uongozi wangu ambayo ni kuimarisha klabu kiuchumi, kupitia App na tovuti hii kunafungua mlango kwa mashabiki na wapenzi wa Young Africans SC kuweza kujisajili kuwa shabiki au mwanachama rasmi, hapo awali tulikuwa tunasajili kupitia fomu za karatasi na taarifa kuhifadhiwa kidijitali ila kwa sasa, utaweza kujisajili moja kwa moja kwa kupitia mifumo hii mipya. Kwa kufanya hivo,itachangia kuongeza mapato ya klabu kwa kupitia ada za usajili na uanachama zitakazotokana na mifumo hii. Ni hatua kubwa na ya kihistoria kwa klabu yetu na itasaidia sana katika kurahisisha utendaji kazi kwa ujumla” Alisema Rais wa Klabu ya Yanga Sc Eng. Hersi Ally Said.

“Hii ni awamu ya pili tuliyoahidi kuanzia mwanzo wa zoezi hili, ambapo sasa wapenzi wa Young Africans SC wataweza kujisajili kuwa Wanachama au mashabiki kupitia tovuti, App na USSD, kwa utaratibu huu mpya tumeshirikiana vyema na wenzetu wa Yanga na N Card ili kuhakikisha kuwa sasa watu wote watakaojisajili waweze kupata kadi zao ndani ya masaa machache, Kwa urahisi huu wa kujisajili na upatikanaji wa uhakika na haraka wa kadi za Wanachama na mashabiki, tunaamini itachangia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo la rais wa klabu na kuimarisha Young Africans SC kiuchumi” Mkurugenzi mkuu wa Kilinet Mohamed Saleh ambayo ndiyo kampuni inayohusika na usajili wa wanachama kwa niaba ya klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala