Connect with us

Makala

Mayele Amponza Yondani

Beki wa timu ya Geita Gold Sports Kelvin Yondani amefungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya kiasi cha shilingi milioni moja kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa Yanga sc Fiston Mayele katika mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya robo fainali uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulioisha kwa Yanga sc kufuzu kwa matuta 7-6 ambapo Yondani alikanyaga Mayele kwa makusudi huku mwamuzi akishindwa kuona tukio hilo ambalo limesababisha kamati ya mashindano ya shirikisho la soka nchini (TFF) Kumfungia beki huyo kwa mujibu wa kanuni namba 41:5:2 inayohusu udhibiti wa wachezaji huku mwamuzi Raphael Ikambi nae akipelekwa katika kamati ya waamuzi kwa kushindwa kuumiliki mchezo baada ya kuwa na maamuzi tata.

Hii si mara ya kwanza kwa Kelvin Yondani kukutwa na matukio tatanishi uwanjani ambapo akiwa katika klabu ya Yanga sc mara kadhaa alikutwa na adhabu za kadi ama faini kutokana na utovu wa nidhamu uwanjani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala