Connect with us

Makala

Mastaa Simba,Yanga sc Watawala Stars

Mastaa wa klabu za Simba sc na Yanga sc wameongoza kwa kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) kilichotajwa kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kimataifa ya kalenda ya Fifa chini ya kocha Kim Poulsen.

Katika kikosi hicho mastaa saba kutoka Simba sc na wengine sita kutoka Yanga sc wameungana na wale wanaocheza soka nje ya nchi pamoja na timu zingine za ndani ya nchi ambazo nyingi zimetoa wachezaji wachache wachache.

Kwa upande wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco ni wachezaji 7  ambao wameitwa ni pamoja na kipa namba moja wa Simba Aishi Manula na mabeki Israel Mwenda, Shomari Kapombe na  Mohamed Hussein huku kwa upande wa viungo ikiwa ni Mzamiru Yassin na Jonas Mkude na mshambuliaji ni mmoja  Kibu Denis.

Yanga sc waliotwa ni Kipa kinda Aboubakary Mshery na mabeki Dickson Job,Bakari Mwamnyeto na viungo ni Zawadi Mauya na Farid Musa pamoja na Feisal Salum Abdallah.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala