Connect with us

Makala

Mashabiki Wawavaa Viongozi Simba sc

Kufuatia sare ya 1-1 iliyoipata Simba sc dhidi ya Mbeya City Fc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya siku ya Jumatano baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wameushukia uongozi wakihimiza ufanye usajili wa wachezaji wazoefu na wenye viwango bora.

Hayo yamekuja baada ya wachezaji watano katika ya saba waliosajili katika kikosi hicho kutofanya vizuri kutokana na kukosa namba ya kudumu wakiwemo Mohamed Outara,Victor Akpan,Nelson Okwa na Nassoro Kapama huku Dejan akiamua kuvunja mkataba na kutimka licha ya kuwa pia alikua hapati nafasi kikosini.

Pamoja na wengi wa mashabiki kupaza sauti kupitia mitandao ya kijamii wakilalamika kuhusu ubora wa kikosi hicho sambamba na viongozi kuitelekeza timu hiyo hasa katika mechi za ndani na hujitokeza katika mechi za kimataifa pekee.

“Mi najua kosa lilipoanzia ila Tusamehe sisi mashabiki ndio tunaoumia champion @moodewji bado mapema ile katiba inayosema sijui mdhamini wa team hawezj kuwa Raisi wa team hapo ndio tulipofeli tumpeni team mazima huyu mwamba uone kama kuna 10 parcent huyu mwamba anajua boli anajua ligi yetu anajua kila kitu kuhusu mpira na anaipenda @simbasctanzania toka moyoni”Aliandika msanii Tundaman katika mtandao wake wa Instagram.
“Hakuna timu isiyofungwa Duniani hiyo ni kweli kabisa Mpira wa miguu Una matokeo 3 kufungwa, kufunga na kudroo hii ni kweli kabisa.Ishu inakuja kwamba timu yako ilicheza vipi kupata Kati ya matokeo hayo matatu?
Najua mpaka sasa hatuwezi kubadilisha hatma ya kikosi chetu Hadi dirisha dogo. Tusikate tamaa tuendelee kuipambania Simba yetu.Hii ndo timu yetu wanasimba hatuna timu nyingine tutakumbushana MAPUNGUFU yetu na tutawaambia viongozi tunataka mabadiliko na maboresho ya kikosi chetu”Aliandika mwanadada anafahamika kama Agness Danny katika mtandao wa Instagram.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala