Connect with us

Makala

Man Utd Yakubali Sare

Klabu ya Manchester United ililazimika kusawazisha kipindi cha pili bao la kujifunga la kiungo wake Fred katika mchezo dhidi ya Southampton katika ligi kuu nchini Uingereza na kuambulia alama moja pekee.

Awali dakika za mwanzoni Southampton walipata bao baada ya kiungo huyo Mbrazil kujifunga huku Man utd wakisubiri mpaka kipindi cha pili dakika ya 54 kusawazisha kupitia kwa Mason Greenwood aliyepokea pasi kutoka kwa Paul Pogba aliyekua na kiwango bora kabisa katika mchezo huo licha ya Man utd kulenga lango mara nne kati ya mipira 15 waliyopiga golini.

Sare hiyo inawafanya United kushuka mpaka  nafasi ya sita ya msimamo wakiwa na alama 4 huku Chelsea na Liverpool wakiwa kileleni kwa alama 6 baada ya kufanikiwa kushinda michezo yao miwili ya ligi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala