Home Makala Yanga Sc Yaifuata Coastal Union Tanga

Yanga Sc Yaifuata Coastal Union Tanga

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha klabu ya Yanga Sc kimeanza safari leo Mei 16  kuelekea Mkoani Tanga leo Asubuhi Mei 16 , 2025 na tayari kimewasili mchana huu kwa ajili ya mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la shirikisho la CRDB dhidi ya JKT Tanzania.

Mchezo huo wa nusu fainali Utakaopigwa Jumapili Mei 18, 2025 katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga majira ya saa kumi jioni.

Katika msafara huo mastaa wote wa kikosi hicho wamesafiri isipokua beki Yao Kouassi ambaye bado ana majeraha ambapo anaendelea na matibabu ya hatua ya mwisho akitafuta utimamu wa mwili.

banner

Taarifa njema kwa Mashabiki wa klabu hiyo ni kurejea kwa Viungo wao Pacome Zouzoua na Khalid Aucho waliokuwa nje ya kikosi kutokana na Majeraha yaliyopelekea kukosekana kwenye mchezo uliopita wa NBC dhidi ya klab ya Namungo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited