Connect with us

Makala

Man Utd Yaanza Upya

Klabu ya Manchester United imeanza upya kusuka kikosi cha msimu ujao baada ya kumtangaza Erik Ten Hag kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Ralf Rangnick ambaye anakuwa mshauri wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao.

Awali Man utd walimleta Rangnick kuchukua nafasi ya Olle Gunnar Solskjaer huku wakimpa jukumu kubwa la kuijenga Manchester United ijayo ambayo itakua na makali uwanjani pamoja na nje ya uwanja kibiashara tofauti na ilivyo sasa.

Hag 52 ameteuliwa kuchukua nafasi hiyo akipewa mkataba wa miaka mitatu huku kukiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi endapo atapata mafanikio huku ikifahamika amewashinda Mauricio Pochetino na Zinedine Zidane ambao nao walikua katika kinyang’anyiro cha kupewa nafasi hiyo.

‘Ni heshima kubwa  kuwa kocha wa Manchester United na nina hamu na changamoto kubwa inayokuja mbele yangu’Alisema kocha huyo ambaye imewagharimu Man United takribani paundi milioni 2 kuvunja mkataba wake na Ajax.

Pia imefahamika kuwa Mitchell van der Gaag ambaye ni msaidizi wake Ajax yuko mbioni kujiunga na kocha huyo kama msaidizi ambapo mpaka sasa mazungumzo yanaendelea kumaliza dili hilo huku pia Steve McClaren akihitajika kurudi klabuni hapo kama msaidizi wa Hag baada ya kuhudumu miaka ya 1999 akimsaidia Sir Alex Ferguson ambapo nae mazungumzo yanaendelea kuja kuunda safu mpya itakayowapeleka mashetani wekundu katika nchi ya ahadi.

Usajili wa kocha huyo kutoka Ajax umekua rahisi kutokana na mahusiano baina ya klabu hizo mbili huku Darren Fretcher na John Murtough wakiongoza mchakato huo na kuvutiwa na kocha huyo kutokana na kuwa na mpango wa muda mrefu huku uwezo wake wa kuwatumia vijana ukiwavutia mabosi hao.

Tangu kuondoka kwa Ferguson mwaka 2013 Man united haijapata mafanikio makubwa licha ya kuajiri waalimu mbalimbali wakiwemo David Moyes,Luis Van Gaal,Jose Mourinho,Solskjaer na sasa Hag akitegemewa kuleta mataji hasa baada ya misimu kadhaa ya kujenga kikosi.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala