Connect with us

Makala

Man Utd Gari Limewaka

Klabu ya Manchester United imekua na matokeo mazuri mfululizo baada ya kufanikiwa kuwachapa Everton 3-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester ikiwa ni mchezo wa kombe la Fa raundi ya tatu ya michuano hiyo.

Ushindi huo ni wa saba mfululizo katika michuano yote iliyocheza siku za karibuni huku ikionyesha mwendelezo mzuri uwanjani huku mastaa wakijitoa ipasavyo kupambania alama tatu ambapo mapema dakika ya nne Antony aliifungia klabu yake goli la kwanza ambalo lilisawazishwa dakika ya 14 na Conor Coady lakini Conor Goady alijifunga dakika ya 52 huku Rashford akiongeza bao la tatu dakika za mwishoni za nyongeza.

Katika mchezo huo Marcus Rashford alionyesha kiwango kizuri huku akifunga katika michezo mitano mfululizo na kumuweka matatani kocha Frank Lampard ambaye licha ya kikosi chake kupoteza pia hakikua katika fomu nzuri huku mashabiki wa klabu hiyo wakichukizwa na matokeo hayo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala