Connect with us

Makala

Feisal ni Mali ya Yanga sc-TFF

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) imeamua kuwa Feisal Salum (Feitoto) ni bado ni Mchezaji wa Yanga SC kwa mujibu wa mkataba aliousaini miaka miwili iliyopita klabuni hapo.

Yanga sc ilipeleka shauri katika Kamati hiyo ikidai kuwa mchezaji huyo hajafuata utaratibu wa kuvunja mkataba hivyo jana pande zote mbili ziliitwa kusikilizwa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, taarifa hiyo imeeleza kuwa uamuzi kamili wa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa Jumatatu, Januari 9, 2023.

Lakini uamuzi wa awali tayari umeamuru kuwa mchezaji huyo bado ni mchezaji halali wa Yanga sc huku Jumatatu ikitarajiwa kuwa kamati hiyo itatoa hukumu kamili pamoja na maelezo kamili ya hukumu hiyo kisheria kutokana na vifungu mbalimbali vilivyotumika.

Kamati hiyo ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisikikiza shauri hilo hapo jana (Januari 6, 2023) pande zote mbili Feisal na Yanga SC waliwakilishwa na Wanasheria wao huku mchezaji huyo pia akifika pamoja na mwanasheria wake ambaye ndie aliyemsimamia Benard Morrison alipokua na shauri dhidi ya Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala