Connect with us

Makala

Man United Yapigwa Chini Kwa Ansu

Barcelona Imekataa Ofa ya euro 150 milioni iliyowekwa Mezani kwa klabu inayodhaniwa,Manchester United kutoka kwa wakala wa Ansu Fati ili kukamilisha usajili wake.

Manchester United ilitarajia kulipa ofa hiyo kwa awamu mbili ikiwa mwanzo euro 125 milioni na baadaye itaongezwa kutokana na kiwango atakachokionyesha,lakini barca imegoma kabisa kuingia kwenye mazungumzo kwa ajili ya kumuuza nyota huyo.

Ansu mwenye umri wa Miaka 17 amerefusha mkataba wake ambao ulitakiwa kumalizika 2022 na sasa unatarajiwa kufikia kikomo mnamo 2024 huku klabu itakayotaka kumnunua baada ya kumaliza muda huo inabidi kuweka euro 400 milioni mezani ili kumpata kinda huyo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala