Ni Azam Fc Tena,Yanyakua Tatu Rukwa

0

Azam Fc imeibuka leo na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu bara uliochezwa uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

Bao pekee la ushindi limepachikwa na Prince Dube dakika 90 kwa kichwa akiwa ndani ya 18 na kufanya kikosi chake kuibuka washindi kwa kujipatia bao la ugenini huku wakinyakua pointi tatu muhimu.

Azam FC inaweka rekodi ya kushinda mechi zake mbili mfululizo ikiwa ugenini baada ya kuanza kushinda mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokone kwa bao 1-0 na leo mbele ya Tanzania Prisons kwa bao 1-0.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.