Connect with us

Makala

Makelele Mbioni Kumrithi Zahera Drc

Mchezaji wa zamani wa vilabu vya Chelsea na Real Madrid Claud Makelele yupo mjini Kinshasa akikamilisha mazungumzo ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kongo kuchukua nafasi ya Florent Ibenge na Mwinyi Zahera.

Kiungo huyo mwenye miaka 46 ni mzaliwa wa Kinshasa japo katika maisha ya soka ameitumikia Ufaransa yupo jijini humo akikamilisha mazungumzo ya mwisho kuchukua nafasi hiyo ya makocha hao wazawa ambao wameshindwa kuipa timu mafanikio katika michuano ya Afcon ambapo timu hiyo ilitolewa katika raundi ya mtoano.

Kiungo huyo aliyezichezea timu za chelsea,madrid na Psg ana uzoefu na ukocha ambapo baada ya kustaafu amewahi kuwa kocha msaidizi wa Pdg chini ya Paul Clement huku akiwa amewahi kuwa kocha mkuu wa timu za Bastia ya Ufaransa na Eupen ya Ubeligiji pia akiifundisha Swasea city kama msaidizi wa Paul Clement kwa mara nyingine huku amewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa klabu ya As Monaco ya nchini Ufaransa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala