Connect with us

Makala

Makazi Mapya Ya Yanga 2020/2021

Bilionea wa GSM ,Ghalib Mohhamed amewahamisha wachezaji wa Yanga pamoja na benchi la ufundi ili kupata utulivu kwenye makazi yao mapya yaliopo Kigamboni kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu bara unaoanza Septemba 6,2020.

Yanga imewekwa kwenye majengo maarufu ya Avic yaliyojitenga na yenye utulivu mkubwa huku ndani yake pakiwemo vifaa vyote vya michezo pamoja na uwanja wa kufanyia mazoezi kwa timu.

Tajiri huyo ameamua kuwaficha huko Yanga Sc ili kuwa kambi yao maalumu na kutofikiria tena suala la hotelini isipokuwa mchezaji atakayejisikia kufanya mazoezi mda wowote awe huru kwani hiyo ndio kambi yao kwa sasa na hakuna mtu yeyote anayewezakuingia pasipo ruhusa au taarifa zake kamili

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala