Connect with us

Makala

Makabi Anukia Yanga sc

Mshambuliaji wa klabu ya Al Hilal ya Sudan ambaye ni raia wa Congo DRC Makabi Lilepo rasmi ameomba kuondoka katika klabu hiyo ya nchini Sudan ili alinde kipaji chake baada ya nchi hiyo kukumbwa na vita hali iliyopelekea michezo kusimamishwa.

Pamoja na kuomba kuondoka,Tayari mchezaji anaviziwa na  klabu za Yanga SC, Azam FC na Simba SC ambazo kwa wakati tofautitofauti zimewasiliana na uongozi wake kuulizia uwezekano wa kupata saini yake.

Tangu msimu uliopita Yanga Sc ilionesha nia ya kumsajili mchezaji huyo lakini ilizidiwa nguvu ya fedha na Al Hilal lakini sasa klabu hiyo ilikua tayari kuwaazima Yanga sc Mchezaji wao ila kwa makubaliano ya mkopo wa Miezi 6 kitu ambacho Uongozi wa Yanga Sc haukuridhia,

Kutokana na sababu hiyo mchezaji huyo amewasilisha barua ya kuomba kuondoka klabuni hapo ili kujiunga na timu nyingine ambapo tayari amethibitisha kupokea ofa kutoka klabu mbalimbali lakini ofa ya Yanga sc ndio iliyomvutia zaidi huku ikitajwa uwepo wa Wakongo wenzake klabuni hapo pia imemshawishi zaidi.
“Nimezungumza na klabu nyingi lakini naweza kusema kuhusu Yanga ndio tuko eneo zuri, nimewaambia ninachohitaji nawasubiri tufikie sehemu tutakubaliana, Yanga ni klabu kubwa wako katika kiwango bora kwasasa, ngoja tumalize majukumu ya timu ya taifa tutajua uhakika ni upi,”alisema Lilepo ambaye ni swahiba wa beki wa Simba sc Henock Inonga
Mpaka sasa kinachokwamisha dili hilo ni mshahara mkubwa anaotaka staa huyo klabuni hapo hivyo bado Yanga sc inasuasua kuhusu hilo ikiomba apunguze kidogo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala