Connect with us

Makala

Mabosi Simba sc Waweka Mzigo Mezani

Mabosi wa Simba wameamua kuifungia kazi mechi dhidi Yanga sc  inayonolewa na Kocha, Nasreddine Nabi baada ya kuamua kuweka mzigo wa maana mezani ili mastaa wa timu hiyo waibuke na ushindi.

Inasemekana kuwa katika kikao cha viongozi wa klabu hiyo kilichofanyika hivi karibuni katika moja ya hoteli kubwa nchini mabosi hao walikubaliana kuweka kiasi cha zaidi ya Sh 300Mil kwa wachezaji ili kufanikisha ushindi jumapili.

Katika mchezo huo, Simba wataingia wakiwa na hasira ya kufungwa mara mbili mfululizo walizokutana katika Ngao ya Jamii msimu huu na uliopita.

Ikumbukwe wakati wa uchaguzi wa klabu hiyo mwenyekiti wa upande wa wanachama wa klabu hiyo Murtaza Mangungu aliahidi kuifunga Yanga sc kama atafanikiwa kuingia madarakani ambapo alishinda uchaguzi huo na sasa ni wakati wa kutekeleza ahadi hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala