Connect with us

Makala

Ligi Kuu Kurejea Februari 1

Bodi ya ligi kuu nchini ( TPLB ) imetangaza mabadiliko ya kurejea kwa michezo ya ligi kuu ( NBC ) kuanzia Februari mosi mwaka huu badala ya Machi mosi ambayo hapo awali ilipangwa baada ya kusogezwa mbele kwa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).

Awali ilibidi ligi kuu irejee baada ya kutamatika kwa michuano ya kombe la mapinduzi na fainali ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ( CHAN ) Ambayo ilipangwa kufanyika kuanzia mwezi ujao katika nchi za Tanzania,Kenya na Uganda.

Baada ya Caf kuamua kusogeza mbele michuano hiyo mpaka mwezi Augusti mwaka huu sasa michezo ya ligi kuu ( NBC ) itarejea juma la kwanza la mwezi wa februari kwa michezo ya viporo kabla ya kuendelea kwa mzunguko wa 17 ambapo tarehe rasmi na ratiba iliyofanyiwa maboresho itatangazwa hivi karibuni .

Michezo hiyo ya viporo inavijumuisha klabu ya Simba Sc ambayo itavaana na Tabora United huku Yanga sc ikicheza na Tabora United.

Bodi ya ligi inatoa wito kwa klabu zote kuhakikisha zinaongeza nguvu katika maandalizi ya timu zao kiufundi pamoja na masuala mengine hasa yanayohusu miundombinu ya viwanja ambavyo vitakaguliwa kabla ya kurejea kwa ligi .

Viwanja vitakavyoonekana kukosa sifa vitaondolewa katika orodha na klabu mwenyeji italazimika kuteua uwanja mwengine miongoni mwa vilivyothibitishwa kwaajili ya michezo yake ya nyumbani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala