Connect with us

Makala

Kumekucha Mbeya City Fc

Kikosi cha timu ya Mbeya City Fc kiko katika maandalizi makali kuhakikisha kinachukua alama zote sita katika michezo miwili iliyobaki ya ligi kuu nchini ili kujihakikishia kutoshuka daraja.

Mbeya city ambayo jumla imecheza michezo 28 mpaka sasa bado ipo hatarini kushuka daraja ikiwa na alama 30 katika nafasi ya 12 na endapo itapoteza michezo miwili iliyosalia basi moja kwa moja itakua hatarini kushuka daraja kama timu za chini yake zitafanya vizuri zaidi katika michezo iliyosalia kwa maana kuna tofauti ya alama mbili pekee.

Katika kuhakikisha hilo uongozi wa timu hiyo kwanza umeandaa mikakati mbalimbali ikiwemo kulipa stahiki zote za mastaa wa timu hiyo pia kuwakusanya mashabiki uwanjani wakati wa mechi kwa kuongeza hamasa kwa mashabiki hao.

Kuhusu suala la kudaiwa na wachezaji Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema wamekuwa wakihangaika sehemu tofauti kutafuta wadau kuwezesha kiuchumi ili kufikia malengo yao huku na kwamba muitikio umekuwa mzuri.

“Niwahakikishie kuwa hakuna mchezaji anayedai timu hadi sasa, tumelipa hadi bonasi za kila mechi kulingana na makubaliano, tunaendelea kujipanga kushinda mechi hizi zilizobaki,” amesema Issa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala