Connect with us

Makala

Kocha Tabora United Kuiwahi Yanga Sc

Afisa mtendaji wa klabu ya Tabora United Charles Obiny ameweka wazi kuwa kocha wao Anicet Kiazmak atarejea nchini hivi karibuni kuiwahi mechi yao dhidi ya Yanga sc inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa nne katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Kwa sasa Kiazmak yupo nchini kwao Congo DR akifanya mafunzo ya kuongeza uwezo [Refresher] kwenye ukocha ili kupanda daraja la juu Zaidi kwa mujibu wa matakwa ya shirikisho la soka barani Afrika (Caf).

“Matumaini yetu hadi kufikia Aprili Mosi atakuwa amejiunga na timu, suala la yeye kufukuzwa kama linavyozungumzwa kwangu halijanifikia ila ninachotambua alituaga anakwenda kufanya kozi yake ya refreshi tu na wala sio vinginevyo”,Alisema Charles Obiny ambaye Afisa mtendaji mkuu wa timu ya Tabora United.

Awali taarifa zilizagaa zikisema kuwa kocha huyo tayari amefukuzwa klabuni hapo huku kukiwa hakuna sababu maalumu baada ya kutoonekana katika michezo kadhaa ya ligi kuu ya nbc nchini.

Kiazmak amepata umaarufu mkubwa nchini kutokana na kuiongoza Tabora United kupata ushindi hasa katika michezo mikubwa ya ligi kuu ambapo alifanikiwa kuzifunga timu za Yanga sc kwa mabao 3-1 na Azam Fc 2-1.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala