Connect with us

Makala

KMC Yazindukia kwa Mtibwa Sugar

Klabu ya Kmc imefanikiwa kuzinduka kutoka usingizini na kuichapa Mtibwa sugar kwa mabao 3-2 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam jioni ya leo.

Awali Mtibwa walianza kupata bao dakika za mapema kupitia kwa George Makan’ga huku Kmc wakisawazisha bao hilo dakika ya 21 kupitia kwa Matheo Anthony lakini Ismail Mhesa aliongeza la pili kwa Mtibwa kwa penati baada ya kuangushwa eneo la 18 dakika ya 41 matokeo yaliyodumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili Kmc walisawazisha dakika ya 73 goli la Hassan Kessy baada ya kipa wa Mtibwa sugar Jeremia Kisubi kupangua vibaya mpira wa faulo huku Matheo Anthony tena akifunga bao la tatu na la ushindi kwa Kmc dakika ya 81.

Kmc sasa wanafikisha alama 27 nafasi ya tisa ya msimamo huku Mtibwa sugar wakiwa nafasi ya kumi na alama 27 pia wote wakiwa na michezo 23.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala