Connect with us

Makala

Kmc Walipa Kisasi Polisi Tanzania

Timu ya Kmc inayomilikiwa na Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni imefamikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam.

Kmc ni kama imlipa kisasi baada ya awali katika duru la kwanza kufungwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika jijini Arusha wailayani Karatu huku mshambuliaji Vitalis Mayanga akiwa mwiba mchungu kwa Kmc siku hiyo.

Katika mchezo huo wa raundi ya pili Kmc ilijipatia mabao kupitia kwa Idd Kipagwile dk 15, Emmanuel Mvuyekule dk 73 na Sadalla Lipangile dk 88 na kuwaacha maafande wakibaki na mshangao wasijue cha kufanya mpaka mechi inamalizika dakika 90.

Sasa Kmc wanapanda mpaka nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu nchini wakiwa na alama 22 huku Polisi Tanzania wakiwa katika nafasi ya tisa wakiwa na alama 19 katika michezo 16 ambayo timu zote zimecheza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala