Connect with us

Makala

Kisa Wasudan,Namungo Wajichia Zanzibar

Namungo FC baada ya kumaliza mechi yake ya ligi dhidi ya Azam FC sasa inaelekeza nguvu zake kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo inajiandaa kucheza na El Hilal Obeid ya Sudan.

Namungo imeenda Zanzibar kujiandaa na mchezo huo ikiwa ni mapendekezo ya kocha Hemed Morocco ambaye anahitaji mechi mbili au tatu za kirafiki.

“Baada ya mechi yetu ya ligi tumegeukia mechi ya Kombe la Shirikisho ambapo tutacheza Disemba 23, 2020 dhidi ya El Hilal Obeid ya Sudan, tutacheza kwenye uwanja uleule wa Azam Complex Chamazi”-Hassan Zidadu, Mwenyekiti Namungo FC.

“Mwalimu amependekeza timu ipate mechi mbili au tatu za kirafiki, tumeangalia ratiba za timu za hapa tumegundua hakuna nafasi kwa timu za ligi kuu wala ligi daraja la kwanza kwa hiyo tumeamua timu iende Zanzibar kwa sababu kuna viwanja vizuri na timu nyingi za kuchezanazo mechi za kirafiki.”

Credit:Shaffihdauda

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala