Connect with us

Makala

Kipigo Brazil Chaondoka na Kocha

Kufuatia kufungwa na Crotia na kuondolewa katika michuano ya kombe la Dunia linaloendelea nchini Qatar kocha wa timu ya Taifa ya Brazil Adenor Leonardo Bacchi maarufu kama Tite ameamua kujiuzuru nafasi ya kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka sita katika nafasi hiyo.

Tite ameamua kuwajibika kuwapisha wengine baada ya kushindwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa Duniani baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-2 dhidi ya Crotia katika mchezo ambao mpaka zikiwa zimesalia dakika sita Brazil ilikua ikiongoza kwa 1-0 ambapo Crotia walifanikiwa kusawazisha na kuja kushinda kwa mikwaju ya penati.

“Mzunguko sasa umefika mwisho na nasimamia maneno yangu,kuna wabobezi wengine wakubwa ambao wanaweza kuchukua nafasi yangu”Alisema Tite mwenye umri wa miaka 61.

Tite anaondoka katika nafasi hiyo akiwa na rekodi ya kuipa timu hiyo taji la ubingwa wa Copa America mwaka 2019 japo alifungwa katika fainali ya michuano ya kombe hilo mwaka 2021 huku akiwa amefungwa katika robo fainali mbili za kombe la dunia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala