Connect with us

Makala

Ureno Waiadhibu Uswisi

Ikicheza bila mshambuliaji bora Duniani Cristiano Ronaldo timu ya Taifa ya Ureno imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Uswisi katika mchezo wa hatua ya mtoani ya 16 bora ya michuano hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Lusail uliopo eneo la Lusail nchini humo.

Katika kikosi kilichoanza mchezo huo kocha wa Ureno Fernando Santos alichukua maamuzi magumu ya kumuweka benchi mshambuliaji staa Cristiano Ronaldo na kumuanzisha Goncalo Ramos aliyefunga mabao matatu huku akionyesha kiwango kikubwa ambapo alifunga mabao hayo dakika za 17,51 na 67 huku Pepe akifunga bao la pili kwa kichwa akimalizia kona ya Bruno Fernandes dakika ya 33 na Raphael Guerrero dakika ya 55 na Rafael Leao dakika ya 90+2.

Uswisi walipata bao dakika ya 58 likifungwa na Akaji aliyemalizia mpira wa kona ambapo sasa baada ya ushindi huo Ureno watavaana na Morocco siku ya Jumamosi kutafuta kuvuka hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa duniani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala