Connect with us

Makala

Kinda Yanga sc Ageuka Gumzo

Kinda wa klabu ya Yanga sc Clement Mzize amegeuka kuwa gumzo mitandaoni baada ya kuiongoza klabu ya Yanga sc kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa klabu hiyo wa ligi kuu nchini dhidi ya Kagera Sugar uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wikiendi iliyopita.

Kinda huyo alipata bao hilo akipokea pasi kutoka kwa Feisal Salum dakika ya 18 ya mchezo bao ambalo lilidumu mpaka dakika tisini za mchezo licha ya Kagera Sugar kujaribu kushambulia mara kwa mara huku pia Uimara wa kipa Djigui Diarra ukwaweka salama wananchi baada ya kupangua penati katikati ya kipindi cha pili.

Mzize ambaye anazitumikia timu zote mbele za Yanga sc ile ya vijana na wakubwa amezaliwa mkoani Tanga a mbapo kwa mara ya kwanza alifika jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanya majaribio katika timu ya vijana ya Yanga sc na kufanikiwa kufuzu moja kwa moja chini ya kocha Mwinyi Zahera.

Kutokana na kufunga bao hilo pamoja na kuonyesha kiwango bora kabisa licha ya kuwa ndio mchezo wa kwanza wa ligi kuu kuanza kwa kinda huyo wadau wengi wa soka wakiwemo waandishi wa habari wamemtabilia makubwa siku za mbeleni hasa kutokana na kupata uzoefu kutoka kwa mastaa kama Fiston Mayele na wengineo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala