Connect with us

Makala

Katwila Arudi Mtibwa Sugar

Sasa ni rasmi kocha Zubeiry Katwila amerudi katika klabu yake iliyomtoa ya Mtibwa Sugar baada ya kuachana nayo miaka mitatu iliyopita na kujiunga na Ihefu Fc yenye makazi yake jijini Mbeya maeneo ya Mbarali.

Awali kabla ya kutambulishwa rasmi kikosini humo kocha huyo alizua gumzo baada ya kuamua kujiuzuru nafasi yake ya ukocha mkuu katika klabu ya Ihefu Fc ambapo taarifa nyingi zilidai kuwa huenda anaweza kujiunga na klabu ya Singida Fountain Gate Fc kama kocha msaidizi.

Sasa ni rasmi kocha huyo ametambulishwa katika klabu hiyo ya Mtibwa Sugar ambapo anatarajiwa kuirudisha timu hiyo katika makali yake baada ya kutokua na mwanzo mzuri katika ligi kuu msimu huu ambapo mpaka sasa wamecheza jumla ya michezo sita wakitoa sare michezo miwili na kupoteza minne wakiwa na alama mbilim pekee mkiani mwa msimamo wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala