Connect with us

Makala

Kaseke Kutua Singida Big Stars

Staa wa klabu ya Yanga sc Deus Kaseke anatarajiwa kujiunga na klabu ya Singida Big Stars mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Inasemekana kuwa Yanga sc haitamuongezea mkataba staa huyo na imepanga kumuaga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City Fc ambapo licha ya klabu hiyo kuhitaji alama tatu kuchukua ubingwa wa ligi kuu nchini.

Yanga sc ilimsajili kaseke akitokea Singida United baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika msimu huo na licha ya kuonyesha kiwango bora msimu uliopita wa ligi akiwa chini ya kocha Cedrick Kaze ambapo alifanikiwa kutengeneza pacha nzuri na Yacouba Songne ambaye hivi sasa ni majeruhi.

Msimu huu Kaseke amekua na wakati mgumu klabuni ambapo kocha Nasreddine Nabi amekua akiwatumia Dennis Nkane,Jesus Moloko na wengine katika winga akimuacha staa huyo nje.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala