Connect with us

Makala

Kaseke Atua Pamba Jiji

Winga wa zamani wa klabu ya Yanga sc na Singida Big Stars Deus Kaseke amejiunga na klabu ya Pamba Jiji Fc kwa mkataba wa miezi sita akiwa kama mchezaji huru.

Kaseke ambaye alikua hana timu tangu aachane na waajiri wake wa zamani ilikua ajiunge na Kengold Fc lakini dili hilo halikukamilika na sasa rasmi amejiunga na Pamba Jiji Fc yenye makao yake makuu jijini Mwanza.

Kocha Fred Felix Minziro ameamua kufanya maboresho katika kikosi hicho akisajili baadhi ya mastaa ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho kueleka duru la pili la ligi kuu ya soka ya nbc.

Kaseke ana uwezo wa kucheza nafasi zote za winga pamoja na kiungo mshambuliaji wa kati lakini pia akiweza kucheza kama beki wa kulia pale inapobidi.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Pamba Jiji ipo nafasi ya 12 ikiwa na alama 12 katika michezo 14 hivyo endapo itaendelea kufanya vibaya basi kukosa nafasi ya kushiriki ligi kuu msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala