Connect with us

Makala

Kapombe,Banda Kuwakosa De Augusto

Beki wa klabu ya Simba sc Shomari Kapombe pamoja na winga Peter Banda wataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Premero De Augosto ya nchini Angola utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi.

Katika mchezo wa awali Simba sc ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 nchini Angola ambapo mastaa hao walikua na majeraha na kuukosa mchezo huo ambapo hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za kupona baada ya kuanza mazoezi mepesi mepesi lakini wanakosa utimamu wa mwili kwa ajili ya mchezo huo.

“Kikosi chetu kimerejea rasmi mazoezini baada ya juzi kurejea kutokea Angola. Kilianza mazoezi jana asubuhi kwenye uwanja wetu wa Mo Simba Arena na leo kitaingia kambini.”
“Tulishinda lakini bado hatujafuzu, safari hii hatutaki kurudia makosa. Tumeweka nguvu kubwa kuona kwamba mchezo wa jumapili tunapata matokeo mazuri ili tuingie makundi. Tumemiss kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”
“Tutaendelea kuwakosa Shomari Kapombe ambaye sasa anaendelea kufanya mazoezi akiwa hospitali, ataukosa mchezo wa jumapili lakini michezo itakayofata atakuwepo. Jimmyson Mwinuke pia tutamkosa, taarifa njema ni Peter Banda amerejea kikosini.”Amesema Meneja habari wa klabu hiyo Ahmed Ally.

Simba sc itakua na kazi rahisi ya kulinda ushindi huo wa ugenini ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki katika hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika ambapo wamefika mara kadhaa huku wakiishia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Tayari mashabiki wa klabu hiyo wameshaanza kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kujaza mashabiki wengi zaidi nchini katika michezo ya kimataifa kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha klabu hiyo uwanjani katika michezo ya hivi karibuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala