Connect with us

Makala

Kamwe Apewa Saa 24 Tabora

Uongozi wa wa klabu ya Tabora United umempa saa 24 Ofisa habari wa klabu ya Yanga Sc Ally Kamwe kumuomba radhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul Chacha Matiko kwa maneno aliyomtamkia katika siku ya Idd Machi 31 2024.

Kamwe alitamka maneno yaliyotafalsiriwa kuwa ya dhihaka na dharau kwa mkuu huyo wa mkoa katika hafla maalumu ya klabu hiyo kula na mashabiki mkoani Tabora.

Kufuatia maneno hayo ya Kamwe,Klabu ya Tabora United imetoa tamko hilo kupitia kwa Christina Mwagala ambaye ni Ofisa Habari wa Tabora United ambapo amesema watalifikisha suala hilo kwa Bodi ya Ligi na TFF kwakuwa kwa mujibu wa miongozo waliyopewa wao kama Maafisa Habari ni kwamba hawajapewa mamlaka ya kuwashambulia Wakuu wa Mikoa bali wamepewa mipaka yao namna ya kufanya hamasa zao.

“Naomba mamlaka husika za mpira wa miguu kwa maana ya TFF na Bodi ya ligi kuchukulia hatua jambo hili, Bodi ya ligi hawajawahi kusema wasemaji tutukane viongozi na nampa masaa 24 Ali Kamwe amuombe msamaha mkuu wetu wa mkoa Paul Chacha”,Alisema Mwagala

Yanga sc na Tabora United zitamenyana siku ya Jumatano machi 2 katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora ambapo katika mchezo wa kwanza Yanga sc ilifungwa mabao 3-1 jijini Dar es Salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala