Connect with us

Makala

Kaizer Yamtosa Nabi

Kufuatia kuweka sharti la kwenda na wasaidizi wake watatu ili ajiunge na klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika ya kusini klabu hiyo imeamua kuachana na kocha Nasredine Nabi na kumuajiri kocha Molefu Ntseki kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

Awali kulikua na mazungumzo ya Nabi kujiunga na klabu hiyo ambapo walikua wameafikiana mambo kadhaa huku ikibaki kumaliza suala la wasaidizi ambapo Nabi alihitaji kwenda na kocha msaidizi,kocha wa viungo na mchambuzi wa mikanda ya video ili wamsaidie katika kuirudishia makali klabu hiyo lakini mabosi wa klabu hiyo walikua wakiweka ngumu wakihitaji kocha wao Arthur Zwane awepo katika benchi la Nabi.

“Taarifa ya ghafla,klabu ya Kaizer Chiefs imefanya maboresho katika benchi la ufundi ambapo tunayofuraha kuwataarifu kuteuliwa kwa Molefi Ntseki kuwa mkuu wa benchi la ufundi kuanzia sasa”ilisomeka taarifa kutoka katika mtandao wa kijamii wa Twitter wa klabu hiyo.

Nabi alihitajika katika klabu hiyo kutokana na kuisaidia klabu ya Yanga sc kufika fainali ya michuano ya kombe la shirikisho huku akifanikiwa kubeba makombe yote nchini katika misimu miwili klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala