Connect with us

Makala

Job,Feitoto Warejea Yanga sc

Mastaa wa klabu ya Yanga sc Dickson Job na Feisal Salum wamerejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu zao za makosa ya utovu wa nidhamu ambazo ziliwafanya wakose michezo ya ligi kuu hasa ule dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumapili.

Feisal alikosa mchezo huo akikabiliwa na adhabu baada ya kuwa na kadi tatu za njano huku ya mwisho akiipata dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kufunga goli kwa kutumia mkono na mwamuzi kuamua kumzawadia kadi hiyo iliyomfanya akakosa mchezo dhidi ya Kagera Sugar ili kutumikia adhabu kwa mujibu wa kanuni.

Kwa upande wa Dickson Job alikosa jumla michezo mitatu kutokana na kufungiwa na bodi ya ligi kwa kosa la kumkanyaga Richarlison Ng’ondya wa Mbeya City katika  mchezo wa ligi kuu zilipokutana timu hizo mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu.

Jumla Job alizikosa mechi dhidi ya Biashara United,Mtibwa Sugar na Kagera Sugar huku klabu yake ikiibuka na ushindi katika michezo yote hiyo huku nafasi yake ikizibwa vyema na Yannick Bangala ambaye mara nyingi huchezeshwa eneo la kiungo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala